Wednesday, 9 November 2011

Jinsi ya kuchagua perfume inayofaa kama zawadi 1


Chrismas na mwaka mpya zimekaribia. kwa kawaida huu ni muda wa ndugu, jamaa na marafiki kupeana zawadi kama ishara ya upendo na kujali. Kama bado haujachagua ni zawadi gani ungependa kumpa umpendaye/unayemjali (awe mama, baba, mke, mme, mfanyakazi mwenzako, ndugu, jamaa au rafiki ) unaweza kuchagua perfume kama zawadi.Kwa nini perfume?
Perfume ni chaguo zuri sana kwa zawadi (iwe chrismas, mwaka mpya, birthday, valentine's day, mother/father's day, kumwambia mtu unampenda/unamjali au kumpa pongezi)kwa sababu ni nzuri, zinatumika kila siku na haisahauliki.

kila mtu anapenda kunukia vizuri na kuvutia. Perfume inamfanya anayeitumia ajisikie vizuri, inaongeza confidence na kuelezea personality ya mtumiaji kama mwanamke au mwanaume. Fikiria kama unaweza kumfanya mtu ajisikie vizuri kwa kumpatia zawadi ya perfume tu. Kwa hakika atakukumbuka kila wakati atumiapo perfume uliyompa na kusiwa na kila anyekutana nae kuwa annukia vizuri. Wonderful!

Kitu kizuri kutumia perfume kama gift ni kwamba haiharibiki mwezi huu au ujao, inaweza tumiwa kila siku na kwa muda mrefu kabla haijaisha na sio rahisi mtu kuisahau uvunguni mwa meza kwani kila mtu anapenda kupamba perfume zake kwenye dressing table yake au sehemu inayoonekana. vilevile mtu hawezi kusema nina perfume za kutosha kwani ni vizuri kuwa na perfume zenye harufubtofauti ili upate ya kazini, kutokea, kushindia nyumbani nk au kunukia tofauti kila siku kuliongana na mood.


Pitia tips za kuchagua perfume ili uweze chagua perfume inayomfaa unayempa zawadi

Endelea kuwepo

No comments:

Post a Comment