Sunday, 23 October 2011

Utajuajee perfume inakufaa



Je wajua kuwa perfume zinaelezewa kama taswira za muziki kwa kuwa zina-notes ambazo kwa pamoja  zinaunda  harufu nzuri ya perfume.  Notes hizi  zimeundwa kwa kutumia utaalam wa mzunguko wa mvuke wa perfume.


Notes za pafume ziko tatu na zinatokea kadri muda unavyokwenda. Unapofungua chupa ya perfume unakutana na note ya kwanza (top note, immediate impression), ambayo inapelekea  note ya pili (deeper middle note) kutokea, hii ni mchanganyiko wa note tpo na base notes. Baadae note ya mwisho ambayo ndio muhimu katika harufu ya perfume inaitwa (base note) inatokea pole pole baada ya nusu saa.



Ni muhimu kuzingatia hizo notes wakati unatafuta perfume itakayonukia vizuri  katika mwili wako. Harufu uinusayo mara baada ya kufungua chupa inaweza kunukia tofauti kabisa baada ya nusu saa ya kujipulizia , hii ni kwa sababu ya mzunguko wa hizo notes za perfume na reaction yake na mwili wako. Ndio maana sio kila perfume inanukia vizuri kwa kila mtu.

 

Kama unataka kujua perfume inanukia vizuri kwenye ngozi yako, pulizia shingoni au kwenye viganja vya mikono kama tulivyoona kwenye older post, acha baada ya nusu saa, halafu jinuse. Kama unaipenda bado hiyo ndio scent yako. Na kama hainukii vizuri kama mwanzo nenda kajaribu nyingine.


Jaribio likifanya kazi, usisahau kurudi humu na kutoa maoni yako.

Karibu tena




No comments:

Post a Comment