Samahani perfumistaz kwa kutoku-update siku mbili tatu zilizopita, majukumu yalikula kwangu kidogo ila sasa nimerudi kuendeleza libeneke kama kawa.
Nimekuja na interesting topic kuhusu muda unaotegemewa chupa ya perfume kuisha. Hata hivyo inategemea unajipulizia spray ngapi kila wakati unapotumia perfume. Pia unaperfume ngapi katika collection yako.
FM 199 100ml for him
Kwa mfano mimi ninapotoka kwenda kazini natumia spray 4. Moja kwenye kila kiganja cha mkono jumla 2 na moja kila upande wa shingo jumla 2. kumbuka hii ni ile kupress na kuachia mara moja (psy) sio ile kupress na kuhold (psyyyyyyyyyy). Nawe pia utakuwa na aina ya upuliziaja wa perfume unaopendelea.
Ukweli ni kwamba kama unaspray perfume kawaida kwenye chupa ya ml 50 kunatakiwa kuwe na wastani wa sprays 735 na 1470 kwenye chupa yenye 100ml.
FM 311 50ml for her
Kwa kuwa kuna siku 365 kwenye mwaka, angalia guideline ifuatayo kujua collection yako ya perfume itachukua muda gani kuisha.
Size ya chupa: Idadi ya spray utumiazo kwa wakati mmoja: Siku zitakazochukua perfume kuisha
50ml 3 245
50ml 5 147
50ml 10 73
100ml 3 490
100ml 5 294
100ml 10 147
Kumbuka hii ni kama unatumia perfume mara moja tu kwa siku, obviously kama unatumia asubuhi na jioni siku zitapungua. na kama una tumia perfume tofauti kila siku siku zitazidi.
Je, ukweli huu umekushangaza? Hii ni sababu nyingine kwa nini kila mtu atumie perfume kwani ni essential kwa matumizi ya kila siku kwa kila mtu smart na zinadumu kwa muda mrefu, what a value for money product to treat yourself, family and friends.
Kama bado, wahi yako sasa stock mpya imeingia. Kuna scent tofauti nyingi kwa hiyo kuna moja kwa kila mtu. wasiliana nasi kama kawaida kupata yako. Bila kusahau wa mikoa ukitoa order leo kesho yake inakuwa delivered.
simu 0716 199 724 au email: imafmtz@gmail.com
Habari nyingi ya kusisimua kuhusu matumizi ya manukato inakuja, usiikose.